Kurugenzi ya Udhibiti Ubora na Masoko
Majukumu
Kurugenzi inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yote yanayohusu ubora na masoko ya tumbaku;
- Kuwasiliana na nchi nyingine za kigeni zinazozalisha tumbaku kama nguvu ya pamoja ya kujadiliana bei katika meza ya mazungumzo;
- Kusimamia shughuli za utangazaji wa tumbaku ndani na nje ya nchi;
- Kuratibu, kudhibiti na kutathmini masoko ya tumbaku ikiwa ni pamoja na utafiti na huduma za ugani;
- Kupanga, kuratibu, na kusimamia utafiti wa masoko na utaratibu wa uuzaji wa tumbaku mbichi;
- Kutunga sheria na kanuni za udhibiti na uhakiki wa ubora; na
- Kusimamia uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya tumbaku katika masoko katika ngazi zote.