Leseni na Vibali
Utoaji wa Leseni na Vibali
Kwa mujibu wa kifungu husika cha Sheria ya sekta ya tumbaku, Bodi ya Tumbaku Tanzania inaweza kutoa leseni na vibali vifuatavyo kwa watu au kampuni iliyosajiliwa:
- Leseni ya Kununua Tumbaku Mbichi Shambani
- Leseni ya Kuingiza Tumbaku Mbichi Nchini
- Leseni ya Kusindika Tumbaku
- Leseni ya Kununua Tumbaku Iliyosindikwa
- Leseni ya Kuuza Tumbaku Iliyosindikwa
- Leseni ya Kusafirisha Tumbaku Nje ya Nchi
- Kibali cha Kuingiza Tumbaku Nchini
- Kibali cha Kusafirisha Tumbaku Nje ya Nchi
Jinsi ya Kuomba Leseni na Vibali
Kampuni au mtu anayetaka kununua, kuuza, kusindika, kuingiza au kusafirisha tumbaku nje ya nchi anapaswa kuomba leseni au / na kibali Bodi ya Tumbaku kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa kutoa leseni na vibali (e-kilimo) kwa kutembelea kiungo hiki: e-Kilimo au kwa kutembelea tovuti ya Bodi na kubonyeza kiungo e-Kilimo.
Mambo yanayoweza kuifanya Bodi kukataa kutoa leseni kwa mwombaji
Bodi inaweza kukataa kutoa leseni kwa mwombaji ambaye:-
- Ameshindwa kuonyesha ushahidi wa uwezo wa kufanya biashara zinazohusiana na leseni anayoomba;
- Kwa mtizamo wa Bodi, mwombaji hawezi kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni;
- Anadaiwa na Bodi, mkulima, mnunuzi au msindikaji; au
- Ameshindwa kuzingatia vigezo na masharti yanayohusiana na leseni iliyotolewa kwake katika msimu uliopita.
Kusimamishwa na Kufutwa kwa Leseni
- Bodi, kwa sababu maalumu zinazojulikana kwa mmiliki wa leseni iliyotolewa, inaweza kusimamisha au kufuta leseni.
- Mtu / kampuni, ambayo leseni yake imesimamishwa au kufutwa na Bodi, haitafanya miamala yoyote ya kibiashara inayohusina na leseni hiyo katika kipindi cha kusimamishwa au kufutwa.
- Mara tu mmiliki wa leseni atakapo rekebisha tatizo lililolazimisha kusimamishwa kwa leseni na baada ya kuisha kwa katazo lililowekwa, Bodi itasitisha kusimamishwa kwa leseni husika.