Kurugenzi ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala
Majukumu
Kurugenzi inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yanayohusu utawala na Mipango na Maendeleo ya Rasilimali Watu;
- Kusimamia kumbukumbu sahihi za rasilimali watu;
- Kusimamia utayarishaji na utekelezaji wa Bajeti ya Mishahara (PE);
- Kusimamia utayarishaji wa taarifa za Rasilimali watu na utawala;
- Kusimamia ajira, uteuzi na upandishaji vyeo kwa wafanyakazi wa Bodi;
- Kusimamia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Nyaraka za Kiutumishi;
- Kusimamia mikataba ya watoa huduma;
- Kusimamia majengo ya ofisi, vifaa na matengenezo yake;
- Kuhakikisha kuwa makato ya kisheria ya wafanyakazi yanalipwa.
- Kusimamia ustawi wa wafanyakazi (ujira, mishahara na marupurupu mengine);
- Kusimamia Tathmini ya Mahitaji ya Mafunzo na maandalizi ya Mpango wa Mafunzo.