Kurugenzi ya Fedha
Majukumu
Kurugenzi inatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yanayohusu Mipango na Usimamizi wa Fedha na matumizi ya Bodi;
- Kusimamia uendeshaji wa shughuli za kifedha za Bodi;
- Kuimarisha usimamizi wa fedha na hesabu;
- Kufanya majumuisho ya bajeti ya mwaka ya Bodi ya matumizi (OC) na Mishahara (PE);
- Kuelekeza na kusimamia utayarishaji wa taarifa za fedha za mara kwa mara;
- Kuimarisha matumizi bora ya mapato ya Bodi katika ununuzi na utoaji wa huduma na vifaa;
- Kufuatilia upatikanaji wa fedha kutoka katika vyombo husika na kusimamia bajeti ya matumizi ya Bodi na kila idara; na
- Kuwezesha ukaguzi wa taarifa za fedha za Bodi.