Matangazo
Tangazo kuhusu kuanza kwa zoezi la tathimini ya zao shambani kwa msimu wa kilimo 2024/2025
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KILIMO
BODI YA TUMBAKU TANZANIA
Bodi ya Tumbaku Tanzania inawatanganzia wadau wote wa tasnia ndogo ya tumbaku nchini kuwa zoezi la tathimini ya zao shambani kwa msimu wa kilimo 2024/2025 linatarajia kuanza rasmi tarehe 17 Februari 2025. Zoezi hili litafanyika kwa muda wa siku 21 mfululizo.
Wadau wote wanakumbushwa kushiriki zoezi hili muhimu kwa ajili ya usatwi wa tasnia. Aidha, Bodi inawakumbusha wadau wote kuhakikisha vitendea kazi muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili vinapatikana kwa wakati. Bodi itatoa ushirikiano mkubwa kwa kupanga ratiba ambayo itazingatia muda na rasilimali za wadau husika.
Idara ya Uendelezaji zao na Uthibiti inawakumbusha Maafisa Kilimo wote wa Bodi katika mikoa yote ya kitumbaku kushiriki zoezi hili kikamilifu ili kuapata matokea makubwa.
IMETOLOEW NA:
MKURUGENZI MKUU
10 FEBRUARI 2025