Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Bodi ya Tumbaku Tanzania

Kurugenzi ya Uendelezaji zao

Majukumu

Kurugenzi inatekeleza majukumu yafuatayo:

  • Kupanga, kuratibu, kudhibiti na kutathmini huduma za uzalishaji wa tumbaku kama vile utaratibu wa Kilimo; Usajili wa mkulima; Kukuza zao; Makadirio ya uzalishaji; Mbinu za usambazaji wa pembejeo; Miundombinu ya uzalishaji; Programu ya Upandaji miti; Siku/mashindano ya wakulima; Uanzishaji na usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya zao; Utafiti wa zao na huduma za ugani.
  • Kupanga, kuratibu, kusimamia na kutathmini huduma za masoko, utafiti na taarifa za masoko, taratibu za kuuza tumbaku mbichi na taratibu za kuuza tumbaku ndani na nje ya nchi.
  • Kupanga na kusimamia huduma za udhibiti wa ubora wa zao ikijumuisha huduma za ukaguzi.
  • Kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya tumbaku katika ngazi ya uzalishaji, usindikaji, ukuzaji na uuzaji.
  • Kuthibitisha na kukagua pembejeo ili kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vilivyoidhinishwa.
  • Kutayarisha na kutekeleza sera za Kurugenzi kwa ajili ya uendeshaji bora wa Kurugenzi na kufikia malengo yaliyowekwa na kuhakikisha kuwa Kurugenzi inafanya kazi ndani ya bajeti ya matumizi iliyoidhinishwa;
  • Kushiriki katika utekelezaji wa mipango mkakati ya Bodi; na
  • Kumshauri Mkurugenzi Mkuu kuhusu masuala yote yanayohusu tasnia ya tumbaku na kupendekeza mipango mikuu ya kisera.