Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Bodi ya Tumbaku Tanzania

Habari


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo yaridhishwa na Ujenzi wa Jengo la Bodi ya Tumbaku Kanda ya Tabora


Kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Philip Mwanyika, mbuge wa Njombe mjini imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Bodi ya Tumbaku Kanda ya Tabora, unaojengwa katika mkoa wa Tabora kwa gharama ya Tsh. bilioni 1.23.

Mhe. Mwanyika ameipongeza Bodi ya Tumbaku kwa kuanzisha mradi huu muhimu, ambao utasaidia katika usimamizi wa zao la tumbaku na kuongeza mapato ya Serikali kupitia upangishaji wa sehemu ya jengo hilo kwa matumizi ya biashara.

Wajumbe wa kamati hiyo, licha ya kubaini kasoro chache katika utekelezaji wa mradi huo, walionesha kuridhishwa na ubora wa kazi iliyofanywa hadi sasa. Kamati imetoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku, Bw. Stanley Nelson Mnozya, kuhakikisha kwamba changamoto zilizojitokeza zinatatuliwa kwa haraka na kwa ufanisi.