Habari
Zoezi la tathmini ya zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025

Zoezi la tathmini ya zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo 2024/2025 imeanza katika maeneo yote yanayolima tumbaku. Madhumuni ya zoezi hii ni kubaini mambo yafuatayo:
- Kiasi cha tumbaku kinachotarajiwa kuzalishwa na wakulima wa tumbaku katika msimu huu;
- Muundo wa mazao unaotarajiwa; na
- changamoto zinazowakabili wakulima msimu huu.
Inatarajiwa kuwa mwisho wa zoezi hii Bodi itaweza kutoa taarifa itakayosaidia wadau wote wa tumbaku katika kupanga msimu wa masoko na msimu ujao wa kilimo wa 2025/2026.