Bodi ya tumbaku Tanzania inayo mamlaka ya kisheria ya kusajili mtu yeyote au kampuni inayotaka kununua, kuuza, na kusindika, kuingiza au kusafirisha tumbaku nje ya nchi. Kampuni au mtu binafsi atatakiwa kutoa taarifa zifuatazo ili kusajiliwa kama mfanyabiashara wa tumbaku yaani mnunuzi, muuzaji, msindikaji, mwingizaji au msafirishaji wa tumbaku nje ya nchi:

  1. Jina na anwani halali ya kampuni au mtu binafsi sambamba na cheti cha usajili wa kampuni;
  2. Leseni halali ya biashara;
  3. Cheti cha namba ya utambulisho wa kodi na cheti cha usajili wa mlipa kodi;
  4. Wanahisa wa kampuni;
  5. Katiba na kanunu za kampuni;
  6. Idadi na sifa za wafanyakazi walioajiriwa;
  7. Taarifa nyingine yoyote kama inaweza kuonekana kuwa muhimu.