RegistrationKwa madhumuni ya udhibiti, wakulima wote wa tumbaku wanatakiwa kusajiliwa na Bodi ya Tumbaku.

Utaratibu wa usajili

 1. Bodi itakuwa na rejista ya wakulima wote wa tumbaku na vituo vya wasaidizi wamiliki, na mameneja wa maeneo yote yatakayopandwa tumbaku na majengo yote yanayotumika au yanayolengwa kutumika kwa ajili ya kupanga madaraja, kukaushia au kufungia tumbaku, vituo vya masoko, maghala na viwanda vya kusindika tumbaku, itakayotunzwa katika namna ambayo Bodi inaona inafaa.

 2. Kila mtu atakayekuwa na nia ya kulima tumbaku kwa ajili ya kuuza ni lazima kwanza asajiliwe na Bodi kabla ya kulima tumbaku.

 3. Kabla ya usajili, mkulima atatoa taarifa zifuatazo kwa Bodi ya Tumbaku:-

  1. Jina la mkulima mwanachama na kama ni chama cha msingi au kikundi, majina ya wakulima binafsi yatatakiwa kuwasilishwa Bodi ya Tumbaku;

  2. Aina ya tumbaku itakayopandwa na maeneo yatakayolimwa katika mwaka huo wa maombi;

  3. Mabani ya kukaushia tumbaku yaliyopo kwa kiasi cha tumbaku kilichokadiriwa kulimwa;

  4. Kiasi cha zao, makadirio ya uzalishaji, hifadhi ya pembejeo na nyongeza ya pembejeo zinazohitajika katika mwaka huo wa maombi;

  5. Hakuna mtu atakayelima tumbaku kwenye eneo lolote la Tanzania bara kwa madhumuni ya kuuza isipokuwa amesajiliwa na Bodi.

  6. Mtu yeyote ambaye atalima au amelima tumbaku kwenye eneo lolote lile ambalo halijatangazwa na Mkurugenzi Mkuu kuwa linafaa kwa ajili ya kulima tumbaku, anatenda kosa kisheria.

Kufuta usajili wa wakulima

 1. Bodi itamwondoa kwenye orodha mkulima yeyote wa tumbaku atakayeonekana kushindwa kukidhi vigezo na masharti ya usajili kama ilivyotolewa katika sheria na kanuni za tumbaku.

 2. Mkulima yeyote wa tumbaku ambaye ana mkataba wenye mikopo ataruhusiwa tu kufuta usajili wake baada ya kutoa taarifa miezi mitatu kabala ya nia yake ya kufanya hivyo.