Chini ya vifungu husika vya sheria ya tumbaku, Bodi ya Tumbaku Tanzania inaweza kutoa leseni zifuatazo kwa watu / makampuni yaliyosajiliwa:-

  1. leseni ya kununua tumbaku mbichi;
  2. leseni/kibali cha kuingiza tumbaku mbichi nchini;
  3. leseni ya usindikaji wa tumbaku;
  4. leseni ya kununua tumbaku iliyokaushwa;
  5. leseni ya kuuza tumbaku iliyokaushwa;
  6. leseni/kibali cha kusafirisha tumbaku nje ya nchi.