valuesIli kufikia dhamira yetu tunaamini katika misingi muhimu ifuatayo ambayo tunajitahidi kuitekeleza nyakati zote:-

Ubora katika huduma

TTB itajitahidi kufikia viwango vya juu zaidi katika utoaji wa huduma, na itakuwa makini kutafuta fursa ya kuboresha viwango hivi.

Uaminifu kwa serikali

Wafanyakazi wa TTB wataitumikia Serikali iliyochaguliwa kihalali, na kutii maagizo halali ya Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bodi ya wakurugenzi, Mkurugenzi Mkuu na maafisa waandamizi wa Bodi kwa uwezo wao wote.

Bidii kazini

Wafanyakazi wa TTB watakuwa katika maeneo yao ya kazi wakati wa saa rasmi za kazi na watakuwa wanajitoa kabisa kwa kazi yao wakati wa masaa ya kazi.

Kutopendelea katika kutoa huduma

TTB haitajihusisha na shughuli za kisiasa katika maeneo ya kazi, au kuruhusu maoni binafsi ya kisiasa kushawishi utendaji wa kazi.

Uadilifu

Wafanyakazi wa TTB hawataomba au kukubali zawadi, upendeleo au vishawishi, fedha au vinginevyo, katika mwenendo utakao athiri majukumu yao. Vivyo hivyo, wafanyakazi hawatatoa zawadi, upendeleo au vishawishi. Aidha wafanyakazi hawatatumia mali za Bodi au muda wa kazi kwa madhumuni yao binafsi na hawatatumia taarifa zilizopatikana katika kutekeleza majukumu yao rasmi ili kupata faida binafsi ya kifedha.

Heshima kwa wote

Wafanyakazi wa TTB watawahudumia wateja na wafanyakazi wenzao kwa usawa. Watajichukulia wenyewe kuwa watumishi wa watu wa Tanzania, na hasa wakati wa kuwahudumia watu wa makundi maalum, kama vile wazee, maskini, wagonjwa, walemavu, na watu wengine wenye mapungufu katika jamii.

Utii wa sheria

Wafanyakazi wa TTB hawatafanya jambo lolote kinyume cha sheria katika kutekeleza majukumu, wala hawatafundisha au kuhimiza mtu yeyote mwingine kufanya hivyo. Kama ikielekezwa kufanya jambo kinyume cha sheria, wafanyakazi watatakiwa kukataa, na kutoa taarifa juu ya suala hilo kwa wakubwa wao wa kazi.

Matumizi sahihi ya taarifa rasmi

Wafanyakazi wa TTB hawatakiwa kuzuilia taarifa ambayo umma una haki ya kupata. Kwa upande mwingine, wafanyakazi hawatatakiwa kutoa au kutumia vibaya taarifa ambayo ni siri.

Kuheshimu jinsia zote

Wafanyakazi watatakiwa kuzingatia masuala ya kijinsia katika kushughulika na wateja na sera, sheria na kanuni.

Utaalamu

Wafanyakazi daima watazingatia maadili na tabia na kutoa huduma ya viwango vya juu zaidi vya kitaalamu.

Uaminifu

Wafanyakazi watakabiliana na wateja kwa njia ya uaminifu na unyenyekevu kuepuka mgongano wa kimaslahi na kutoa taarifa yoyote kamili inayohitajika.