Historia ya kilimo cha tumbaku (Nicotiana tobaccum) nchini inarudi nyuma miaka ya 1930, wakati zao la tumbaku lilipoanzishwa kwa mara ya kwanza wilaya ya Songea likitokea Nyasaland (Malawi). Uanzishwaji wa kilimo cha tumbaku wilayani Urambo katika mkoa wa Tabora baada ya Vita ya pili ya dunia (1940) ndio ulikuwa mwanzo wa maendeleo ya kilimo cha tumbaku nchini.

Tangu wakati huo, zao la tumbaku limekuwa tegemeo la jamii katika nchi yetu na hadi sasa tumbaku inazalishwa katika mikoa 13 ya kiutawala inayojumuisha wilaya 33.

 1. Tabora (Urambo, Manispaa ya Tabora, Uyui, Nzega, Sikonge na Kaliua)
 2. Katavi (Tanganyika, Mlele and Mpanda);
 3. Shinyanga (Kahama);
 4. Geita (Chato, Geita, Mbogwe and Bukombe);
 5. Kagera (Biharamulo);
 6. Kigoma (Uvinza, Kasulu, Kakonko and Kibondo);
 7. Iringa (Manispaa ya Iringa, Mfindi)
 8. Singida (Manyoni);
 9. Mbeya (Chunya);
 10. Ruvuma (Songea Vijini, Namtumbo, Mbinga na Tunduru);
 11. Songwe (Wilaya ya Songwe);
 12. Mara (Serengeti, Tarime and Rorya) and
 13. Morogoro (Kilosa).